Na Allan Ntana
WATU 3 wanaomiliki maduka ya dawa mkoani Tabora wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora kwa makosa ya kusababisha kifo cha mwanamke mjamzito aitwaye Esta Chimika na mtoto aliyekuwa tumboni kwa kujifanya wahudumu wa afya na kumzalisha mwanamke huyo kisha kumsababisha kifo.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora Jovita Kato wakili wa serikali mwandamizi Juma Masanja amesema katika shitaka la kwanza mnamo Machi 15, 2020 majira ya saa tisa mchana.
Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Ezekiel Kazimoto Masanja,Victoria Boniface Makamba na Regina Florence Balaye wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa tabora na kusomewa mashitaka mawili ya mauaji.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walisababisha kifo cha Ester Chimika baada ya kujifanya wahudumu wa afya (waganga) na kumzalisha mwanamke huyo katika kijiji cha miswaki halmashauri ya wilaya ya Uyui, ambapo katika kosa la pili wanashitakiwa kwa kuharibu mtoto ambaye angezaliwa akiwa hai na makosa yote ni kinyume cha kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.
Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo na wamerudishwa mahabusu hadi tarehe 14/4/2020 kwa ajili ya kutajwa tena.
More Stories
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango
Ujenzi miradi ya maendeleo umebadilisha maisha wananchi Katavi