November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maamuzi kesi ya Yanga, Morrison sasa ni Agosti 24

MAHAKAMA ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jana imemaliza kusikiliza kesi ya kati ya klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji wao wa zamani Benard Morrison anayedaiwa usajili wake ndani ya klabu ya Simba kutofuata taratibu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na klabu ya Yanga mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo namba CAS2020/A/7397, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka Agosti 24, 2021.

Yanga ilingii kwenye sintofahamu na nyota huyo mwaka jana jambo lililofanya kupeleka kesi katika Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ambayo iliketi kwa takribani siku tatu hadi kumaliza sakata hilo.

Maamuzi yaliyotolewa na Kamati baada ya uchunguzi wa nyaraka mbalimbali na kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ulimuweka huru mchezaji huyo ambaye alijiunga Simba baada ya kutakiwa kuchagua timu anayotaka kuitumikia lakini akipewa masharti ya kurudisha kiasi cha fedha alichokichukua kwa viongozi wa Yanga.

Kitendo cha Kamati kutoa maamuzi hayo hakikuwafurahisha upande wa Yanga ambao waliamu kutaka rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) ili kupata nafasi ya shauri lao na Morrison kusikilizwa upya wakiamini haki yao juu ya mchezaji huyo itapatikana.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Yanga iliibuka upya sakata hilo na kudai tayari walishalipa malipo ya awamu ya kwanza ya shauri na lilishasikilizwa na walichokuwa wakisubiri kupata majibu ni hatua gani inayofuata.

Desemba Yanga walipokea barua kutoka CAS iliyowataka kwa pamoja kulipa fedha za Ufaransa ambazo ni 12,000 jumla 24,000 kabla ya Januari 12 ili jaji aweze kuendelea na shauri lao.

Alipokuwa akitolea ufafanuzi sakata hilo, Februari mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliliambia Majira kuwa, walishalipa fedha hizo na tayari Morrison alishaonekana na kesi ya kujibu na kutakiwa kujieleza kupitia kwa wanasheria wake.

Baada ya kupita miezi kadhaa, klabu ya Yanga juzi imetoa taarifa rasmi ikidai kwa muhibu wa sheria na taratibu za uendeshaji wa mashauri wa CAS hawakuruhusiwa kutoa mwenendo wa kesi hiyo mpaka itakapotolewa maamuzi.

Taarifa hiyo iliweka wazi kuwa, kilichochelewesha kesi hiyo ni pingamizi la awali la CAS kusikiliza rufaa hiyo iliyowekwa na Morrison aliyetaka keshi hiyo kurudishwa hapa nchini.

“Baada ya Mahakama hiyo kusikiliza hoja za pande zote mbili juu ya pingamizi, CAS imelitupilia mbali pingamizi hilo Juni 2, 2021 walianza rasmi kusikiliza kesi ya msingi huku pande zote mbili zikitakiwa kuwasilisha taarifa ni kwa namna gani kesi hiyo itasikilizwa kwa kutuma nyaraka au kwa njia ya maneno,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa CAS keshi hiyo iliyosajiliwa kwa namba CAS2020/A/7397 ikiwa na maana kesi ya 7397itasikizwa leo na huenda pia maamuzi yakatolewa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo, uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake.