
Na Israel Mwaisaka, Majira online, Nkasi
Mkuu wa Wilaya Nkasi Peter lijualikali amesema kuwa asilimia 70 ya kero zote zilizowasilishwa kwa Waziri mkuu katika ziara aliyoifanya hivi karibuni zimetafutiwa ufumbuzi.
‎Akizungumza leo ofisini kwake amesema kuwa Kuna kero nyingi ambazo ziliwasilishwa na ofisi yake ilipewa jukumu ya kuzishughulikia na kuwa nyingi zimefanyiwa kazi na kufikia ukomo huku nyingine likiendelea kutafutiza ufumbuzi.
‎Amedai kuwa licha ya kero zilizowasilishwa mbele ya Waziri mkuu pia ofisi yake imeendelea kupokea kero mpya kutoka kwa Wananchi huku nazo zikitafutiwa ufumbuzi wa kina .
‎Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuwa zipo baadhi ya kero utatuzi wake ni mrefu kwa maana ya kupelekwa katika wizara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi hizo zinachukua muda kidogo lakini kwa zile ambazo utatuzi wake ni hapa hapa wilayani wanamaliza kwa wakati.
‎Pia aliwasihi Wananchi kuwa wakweli wakati wa kuiwasilisha kero mbele ya viongozi kwani wapo baadhi ya Wananchi walisema uongozi kitu ambacho si kizuri lakini amewataka Wananchi wenye kero kuendelea kuziwasilisha ofisini kwake na kutafutiza ufumbuzi.

More Stories
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni