Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kassim Majaliwa leo ametangaza Ofa ya tiketi na usafiri kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wote wanaoshiriki kikao kazi Cha 18 kwenda Uwanjani kuishangilia Taifa Stars.
Stars itajitupa uwanjani kesho dhidi ya Uganda ‘The Cranes’, mchezo utakopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo wa kufuzu AFCON 2023.
Majaliwa ametangaza ofa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa a Michezo kwa Maafisa hao, wakati akifungua kikao kazi cha 18 cha
Maafisa hao kinachofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara Said Yakubu ameshiriki.
Taifa Stars itacheza na Uganda The Cranes kesho ikiwa ni mechi ya marudiano baada ya kuifunga Goli 1 Kwa 0 katika mchezo wa awali uliochezwa Machi 24, 2023 mini Ismailia nchini Misri.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM