Na Judith Ferdinand,Meatu
SERIKALI ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepanga kujenga maabara 10 za kupima magonjwa ya mifugo kupitia bajeti ya 2020/2021 ili kudhibiti ueneaji wa magonjwa ya mifugo(wanyama) nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Meatu Mkoani Simiyu ya kukagua ukarabati na ujenzi wa josho la kuoshe mifugo la Kijiji cha Mwakisandu na Isangijo, ujenzi wa maabara na kliniki ya mifugo ya Halmashauri ya Meatu pamoja na shughuli ya ukuzaji wa vifaranga vya kuku kijiji cha Mwandoya.
Ulega amesema,lengo la Serikali ni kuhakikisha inapunguza kwa kiasi kikubwa ueneaji wa magonjwa ya wanyama na kuyadhibiti kwani wanataka kuhakikisha wafugaji nchini wanawahudumia kwa ukaribu.
Kwa sasa wana Kanda ya Masharik,Kaskazini,Magharibi na Kanda ya Ziwa ,lakini wanataka waongeze ili huduma hiyo isogee karibu zaidi na kwa msingi huo uzalishaji wa chanjo zile za kipaumbele mpaka sasa wamefanikiwa kuzalisha chanjo sita hapa nchini.
“Chanjo hizo ni za mdondo,kutupa mimba,chambavu,vilevile tuna ya pamoja chambavu na ya kutupa mimba na chanjo ya homa ya mapafu ya ng’ombe (CBPP) hii ni chanjo ya karibuni ambayo inaendana na mazingira ya hapa kwetu tofauti na zile za nje ambazo zinahitaji jokofu kuzitunza,” amesema na kiongeza kuwa
Amesema harakati za kuogesha mifugo zinakwenda vizuri ambapo mwaka 2017/2018 wamenunua chanjo ambazo wametoa ruzuku kwa halmashari nchini za milioni 300 lita takribani 8,000 huku mwaka 2019/2020 serikali imenunua tena lita 12,000 ambayo ni karibu milioni 400 ambazo wamezileta kwenye halmashauri na sasa wafugaji watakwenda kuogesha ng’ombe mmoja kwa shilingi 50.amesema
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja