January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lushoto DC yapokea magari mawili ya wagonjwa,pikipiki sita

Na Yusuph Mussa, Timesmajira Online, Mwanza Lushoto

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Ikupa Mwasyoge amesema wamepata magari mawili ya wagonjwa kwenye Kituo cha Afya Mlalo na Mtae.

Pamoja na pikipiki sita kwa ajili ya huduma za afya kwenye Hospitali ya Wilaya Lushoto, Kituo cha Afya Mlalo, Kangagai, Mtae, Mlola,zahanati ya Manolo na Mng’aro.

Mwasyoge amebainisha hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo huku akieleza kuwa mbali na vyombo hivyo vya usafiri pia wamepata jokofu nane (8) kwa ajili ya kutunzia sampuli za damu na Centrifuge machine kwa ajili ya kuchakata sampuli.

Ambapo ameeleza kuwa vitu hivyo vitaboresha huduma za afya kwenye halmashauri hiyo.

Majokofu hayo yanapelekwa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, Kituo cha Afya Mlalo, Mlola, Mtae na Kangagai pamoja na zahanati ya Mng’aro, Sunga na Manolo.