Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Tunduma.
WATU watano, wakiwemo watatu wanaodhaniwa kuwa ni wa familia moja wamefariki kwenye ajali iliyosababishwa na lori lililobeba bia kufeli break na kugonga gari dogo na Bajaji katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) eneo la mteremko wa mlima Chengula Mjini Tunduma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameeleza kuwa imetokea Oktoba 17, 2023, majira ya saa 9:30, ambapo lori hilo la mizigo lililokuwa likitokea mjini Tunduma kuelekea Mbeya likiendeshwa dereva asiyefahamika na ambaye alikimbia baada ya ajali kutokea.
Kamanda Mallya amesema kuwa, lori hilo lenye namba T.468 BUM na tela lake T 262 CBR aina ya Scania baada ya kufeli breki liligonga gari dogo lenye namba T 500 DWN aina ya Toyota Vanguard lililokuwa likiendeshwa na Elikana Kayungilo (38) Mkazi wa Vwawa kisha kwenda kugonga Bajaji namba MC 574 DLW aina ya TVS iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye hajafamika na amefariki papo hapo.
Amesema pia abiria wote watatu ambao wanadhaniwa kuwa ni wa familia moja waliokuwa kwenye bajaji hiyo walipoteza maisha na kutaja majina yao kuwa ni Faustina Hala (50) , Vicent Mapunda (25) , pamoja Venance Faustini (25) ambao anadaiwa kuwa ni mapacha waliokuwa wakijishghulisha na kazi za ufundi selemala, wote wakiwa ni wakazi wa Mpemba, Mjini Tunduma.
Aidha, Kamanda Mallya amesema marehemu wengine wawili ambao ni dereva wa bajaji na utingo wa lori hawajatambuliwa na miili yao imehifadhiwa katika kituo cha afya Tunduma.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi