March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Latifa achukua fomu ya Udiwani Majohe

Na Heri Shaaban,Timesmajira Online-Dar

MWENYEKITI Mstafu wa mtaa wa Kichangani ,Latifa Kimaro,amejitosa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Udiwani kata ya Majohe wilayani Ilala mkoa Dar-es-Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari,mara baada ya kuchukua fomu,amesema wananchi wa Majohe wamempa baraka za kugombea nafasi ya Udiwani baada ya kuona anatosha kutumikia kiti hicho.

“Katika uongozi wangu wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kichangani, nimetekeleza ilani kwa kufanya maendeleo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,afya huku kwenye maji ametekeleza kwa asilimia 75,hivyo huduma zote za kijamii zinapatikana,amesema Latifa.