March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kumbilamoto achukua fomu ya Udiwani Vingunguti

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online-Dar es Salaam

Omary Kumbilamoto amechukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Udiwani katika ofisi ya Kata ya Vingunguti kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), kwa ngazi ya Diwani katika Kata hiyo.

Kumbilamoto ambaye alisindikizwa na umati wa wananchi na wanachama wa ccm Vingunguti majira ya saa 9:40 asubuhi pamoja na viongozi wa kata

Mara baada kuchukua fomu hiyo Kumbilamoto,amesema kipindi kilichopita alikuwa Diwani wa Vingunguti pia Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam, ambapo ametekeleza kwa vitendo mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

Aidha amesema katika miaka mitano ya Udiwani amewezesha kupatikana kwa gari ya kubeba wagonjwa(Ambulance),katika zahanati ya Vingunguti, soko la kisasa la nyama choma, machinjio na mabucha ya kisasa pamoja na barabara za zege mitaani .