January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kuhudumia wateja na utoaji wa taarifa kwa wakati vyaipa tuzo TANESCO

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeshinda tena tuzo kutoka Jamii Forums kwa utoaji majibu ya changamoto za wateja kwa wakati ,kuzifanyia kazi pamoja na utoaji wa taarifa mbalimbali.

Kupitia ukurasa hai (Thread ya TANESCO) inayoendeshwa kwenye Jukwaa la Jamii Forums, Tanesco wamekua wakijibu na kutoa suluhisho la matatizo mbalimbali ya wateja wanapopata changamoto za upatikanaji wa umeme Nchini.

Tuzo hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita zikihusisha taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na Viongozi walio mstari wa mbele kwenye kutatua kero za Wananchi kupitia mitandao ya Kijamii kwa haraka kadri zinavyojitokeza.