Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uthibiti ubora mashuleni wakiimba wimbo wa Taifa mara tu baada ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Profesa Carolyn Nombo, kuingia kumbini kwa ajili ya kufunga mafunzo ya siku tatu ambayo yametolewa na Wizara kwa walimu zaidi ya 11,850 nchini.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Profesa Carolyn Nombo akifunga mafunzo ya uthibi ubora mashuleni kwa walimu wakuu wa shule na waratibu elimu kata wa halmashauri zote mbili za Wilaya ya Songea. Mafunzo hayo ambayo yametolewa na Wizara ya elimu yamelenga kuzijengea uwezo juu ya utekelezaji wa majukumu yao.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Wlimu Profesa Carolyn Nombo akiwapungia mkono washiriki wa mafunzo ya uthibiti ubora wa elimu mashuleni, ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwa walimu wakuu wa shule na waratibu elimu kata wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Zaidi ya walimu 11 850 wamepatiwa mafunzo hayo nchini. Picha zote Cresensia Kapinga.
More Stories
Kituo cha mfano Katente chaongeza makusanyo MBOGWE
Elimu ya fedha yawafikia wananchi wa Makanya wilayani Same
Wasira:Uchaguzi Mkuu utafanyika wanaCCM,Wananchi jiandaeni