January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kocha Robetinho atimuliwa Simba SC

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho), sambamba na kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC leo, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, klabu hiyo inawashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu hiyo na kuwatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Aidha, Simba SC imethibitisha kuwa kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola katika kipindi hichi cha mpito huku mchakato wa kutafuta makocha wapya ukitarajiwa kukamilika hivi karibuni.