January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KMC washusha kifaa kipya kutoka Yanga

Klabu ya KMC imeendelea kujiimarisha baada ya kumnasa aliyekuwa beki wa klabu ya Yanga Andrew Vicent maarufu kwa jina la Dante. Beki huyo mahili aliachana na Yanga baada ya mkataba wake na klabu hiyo kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

Dante amepata dili la mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mkoani kinondoni jijini Dar es salaam. Dante anategemewa kuwa nguzo muhimu kwa klabu hiyo kutokana na uzoefu wake ndani ya ligi kuu Tanzania bara.