November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiwila City yaibuka mshindi katika Michuano ya Tulia Trust  Cup 2021

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Rungwe.


TIMU ya mpira wa miguu ya Kiwira city imetwaa ubingwa wa ligi yakombe la Tulia trust 2021 kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3 kwa 1dhidi ya Katabe fc baada ya kutofungana katika kipindi cha dakika 90
za kawaida.

Mtanange huo ulipigwa jana katika viwanja vya Tandale Tukuyu Wilaya yaRungwe mkoani Mbeya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi waTaasisi ya Tulia Trust, Dk. Tulia Ackson  ambaye pia ni Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Timu ya Kiwira City ilitinga hatua ya fainali baada ya kuiondoa timuya Igogwe kwa jumla ya magoli 4 kwa 2 huku Timu ya Katabe fc ikiitoatimu ya Bulyaga fc kwa goli moja kwa nunge.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Dk. Tulia amesemaligi hiyo itakuwa endelevu kwa kila mwaka lengo likiwa ni kuinuamichezo kwa vijana ambapo alitoa wito kwa timu zingine kuendeleakijifua Zaidi kwani mashindano yajayo yatashirikisha timu nyingiZaidi.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Afisa Michezo Wilaya ya Rungwe, EnziSeme amesema kutokana na uwepo wa maambukizi ya Uviko 19 maandalizi ya ligi hiyo yalichelewa hivyo kupelekea timu zilizoshiriki kuwa chache
na kuanzia hatua ya 16 bora.

Amesema  ligi hiyo ni muhimu kwa Wilaya ya Rungwe kwani licha ya kuinua sekta ya michezo pia vipaji vya vijana huonekana na kuwawezesha kuonekana na timu kubwa na kuwapatia ajira.

Katika ligi hiyo, mshindi wa kwanza Timu ya Kiwira City ilijinyakulia kikombe Pamoja na fedha taslimu shilingi milioni moja zilizotolewa na Mbunge wa Rungwe, Anton Mwantona  huku mshindi wa pili Timu ya Katabe
ikijinyakulia shilingi Laki tano(500,000/=).

Timu ya Bulyaga iliyoambulia nafasi ya tatu ilipata shilingi 300,000/=
huku zawadi zingine zikienda kwa mashabiki bora waliopata shilingi 100,000/= ambao wanatoka timu ya Kiwira city,  mwamuzi bora ni Lucy Mwamfupe, mfungaji bora Anord Mtewele kutoka Katabe fc na Mlindamlango
bora akiwa ni James Steve kutoka Igogwe fc wote wakijipatia shilingi laki moja kila mtu.