December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiwanda MSD Idofi kuokoa bil. 33/- kwa mwaka

Na Zena Mohamed, TimesMajira Online, Dodoma

BOHARI ya Dawa (MSD) inataokoa matumizi ya fedha za kigeni kiasi chash. bilioni 33 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununu mipira ya mikononje ya nchi kutokana na kuwa hatua za mwisho za ukamilishaji wamiundombinu ya kiwanda cha mipira mipira hiyo kilichopo Idofi, mkoaniNjombe.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma jana na Meneja Mipango, Ufutiliaji naTathmini wa MSD, Hassan Ibrahim, wakati akizungumza na waandishi wahabari kuhusu utekelezaji wa shughuli na mafanikio ya MSD.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Ibrahim amesemakiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi ujao (Septemba, mwaka huu)na kinatarajiwa kuzalisha takribani jozi 86,400,000 za mipira yamikono kwa mwaka na kitachagiza uzalishaji wa malighafi ya mipirakutoka maeneo tofauti nchini.

“Uzalishaji huu utapunguza utegemezi wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchina kuokoa matumizi ya fedha za kigeni, lakini kiwanda hiki pia kitatoaajira za moja kwa moja kwa Watanzania takribani 200,” amesema nakuongeza;”Jukumu hili la uzalishaji litafanyika kupitia Kampuni Tanzu ya MSDiitwayo ‘MSD Medipharm Manufacturing Company LTD’ ambayo imesajiliwarasmi Aprili 2023, Kampuni hii itaongeza ufanisi na kutoa fursa yakushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji wa bidhaa za afya.”

Aidha, Ibrahim amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa kiasicha sh. bilioni 157.56 katoka mwaka wa fedha 2022/23 kwajili yaununuzi wa bidhaa za afya za vituo vya afya vya kutolea huduma zaafya.

“Kiwango hiki cha sh. bilioni 157.56 ni kiwango cha juu kuwahikutolewa na Serikali kupitia MSD tangu kuanzishwa kwake miaka 30iliyopita,” amesema.

Amesema Serikali kupitia MSD imeanza rasmi kutekeleza jukumu lausambazaji wa bidhaa za afya mara sita badala ya mara nne kwa mwakakwa vituo vyote vya umma vya kutolea huduma za afya kwa mwaka wa fedha2022/23.

Kwa mujibu wa Ibrahim hatua hiyo imetokana na mapitio ya mnyororo waugavi na mapendekezo ya maboresho ya usambazaji bidhaa za afya.

Amesema usambazaji huo umeondoa changamoto za upatikanaji wa bidhaa zaafya ukilinganisha na mfumo wa awali wa kusambaza kila baada ya miezimitatu sawa na mara nne kwa mwaka.