Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Timu ya Jumuiya ya Wazazi ya chama Cha Mapinduzi CCM Kivule imeibuka mabingwa katika mashindano ya mpira wa miguu kwa kuifunga timu ya Kitunda kwa mabao 2 – 0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Misitu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ngazi ya mkoa ambapo timu zinashindana kuanzia ngazi ya kata, jimbo, wilaya na baadaye mkoa.Mabao ya Kivule yalipatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili ambapo wakati wote walionekana kutawala mchezo huo.
Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Kivule, Reuben Mduma, alisema timu ya Kivule itaungana na timu nyingine zilizoshinda katika kanda mbalimbali za Jimbo la Ukonga kisha kuchuana kupata timu zitakazowakilisha ngazi ya jimbo.
“Wanachama wamehamasika, tunaibua vipaji mbalimbali, washindi wataunda timu za majimbo kisha wilaya na baadaye tutapata timu ya mkoa,” alisema Mduma.
Naye Katibu Mwenezi Kata ya Kivule, Hemed Pogwa, alisema mashindano hayo yanawaleta wanachama pamoja na kuongeza hamasa na umoja katika chama hicho.
Hemed aisema pia kupitia mashindano hayo kazi ya kufikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi inakuwa rahisi zaidi.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania