November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kim: Tunaanza safari kuijenga Taifa Stars Juni

Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen amesema kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitaingia kambini mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia.

Awali michuano ilitakiwa kuanza kutimua vumbi Juni lakini Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) imetangaza kuisogeza mbele michuano hiyo ambayo sasa itaanza Septemba, Oktoba na Novemba.

Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano maalum na televisheni ya TFF TV, kocha huyo ameweka wazi kuwa baada ya FIFA taarifa ya mabadiliko hayo wanachokisubiri sasa ni kupata taarifa zaidi huku wakiendelea na maandalizi.

Amesema, kambi hiyo itadumu kwa takribani siku 10 kwani wanahitaji maandalizi ya mechi zao za kirafiki ambazo kwa mujimu wa kalenda ya FIFA mechi hizo zitachezwa kati ya Mei 31 hadi Juni 15, 2021.

Kocha Kim amesema kuwa, katika hatua hiyo ya kwanza wanatarajia kucheza mechi moja au mbili za kirafiki na baada ya Ligi kumaliza huanda wakawa na kambi nyingine mwezi Agosti ambayo itadumu kwa wiki kadhaa ikiwa ni hatua ya pili kwani wanahitaji zaidi muda wa mazoezi ya pamoja iki kujenga kikosi imara chenye muunganiko mzuri.

Itakumbukwa kuwa mara baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), kocha huyo aliweka wazi anayachukulia matokeo hayo sehemu katika safari yake ya kujenga Taifa Stars imara na yenye nguvu.

Kim amesema kuwa, mikakati ya benchi lao la ufundi ni kwenda kuunda Taifa Stars imara itakayokuwa bora kwenye mipira, itakayokuwa vizuri kwenye pasi na kucheza ndani ya falsafa bora kwani kwa asilimia fulani vijana wake walimuonesha kuwa ikiwa wataweka nguvu kubwa katika eneo hilo basi itakuwa rahisi kujua namna wanavyohitaji kujinda na vipi wanataka kushambulia.

“Ili kufanikiwa katika soka ni lazima ujue jinsi ya kutumiza vizuri mudahivyo licha ya kusogezwa mbele kwa mashindano haya lakini tutatumia muda huu kwa ajili ya kuanza maandalizi hivyo Juni kikosi kitaingia kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi,”

“Mwezi Agosti tutafanya mazoezi ambayo yataanza kutuweka tayari kwa ajili ya mechi hizo za kufuzu kucheza kombe la Dunia ingawa hadi sasa bado hatujajua tutacheza wapi na nani hadi pale itakapotoka ratiba ya CAF,” amesema kocha Kim.

Kocha huyo alisema kuwa, kuna v itu anahitaji kuvibadili ndani ya timu yake ambavyo vyote vitafanikiwa katika uwanja wa mazoezi na ndio maana wa mepanga kuitumia vizuri kambi ya mwezi Agosti ambayo itakuta Ligi imeshamalizika kuweka kambi kwa takriban wiki tatu.

“Kwa asilimia kubwa kambi hii itasaidia benchi la ufundi kujua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na jinsi watakavyocheza kwa ushirikiano kwani tunachotaka ni kuona kila mmoja anakuwa bora katika nafasi yake kwani ili kuweza kushinda ni lazima uwe na maandalizi bora,” amesema kocha huyo.