Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SERIKALI imekemea Watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia uliyofanyika jana Januari 27. 2024 nchini huko.

Waziri amesema uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Saudi Arabia hauruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila kufuata utaratibu, hivyo kila Mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili.

Kikwete amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa Watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa afya, kupata kazi zenye staha na mshahara mzuri ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.

More Stories
Serikali yaweka mazingira rafiki kuvutia uwekezaji sekta ya elimu
Mixx yakabidhi zawadi kwa washindi watatu Sabasaba
Serikali yaahidi kuendelea kuunga mkono Wawekezaji wa Usafiri wa Umeme