May 12, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikwete:Uwekezaji kwenye rasilimali watu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi

Na Penina Malundo,Dar es Salaam

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete, amesema nchi ili iweze kuendelea ipo haja ya kuwekeza kwenye rasilimali watu, kwa kuwaendeleza katika elimu kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu, bila kusahau mafunzo ya ufundi.

Kikwete aliyasema hayo leo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu SabaSaba, amesema nchi yeyote duniani iliyoendeleza kwa watu wake, kwa kuwaendeleza kielimu kwa ngazi ya chini hadi ya juu.

“Vyuo vikuu kazi yake kufundisha na moja ya kazi kubwa ni nchi kuendeleza rasilimali watu kupitia elimu ya msingi sekondari hadi vyuoni na vya mafunzo Ufundi,”amesema na kuongeza

“Nikiwa Wizara ya Mambo ya Nje, nilikuwa na kauli mbinu ‘Tunafanya vizuri kuliko Jana’ hii ilikuwa kauli mbiu wakati huo. Yaani tuwekeze zaidi. Nimepita banda la UDSM nimeona ufumbuzi kwa kutumia rasilimaili zinazozaloshwa nchini, kwa kutengeneza bidhaa,” amesema Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho.

Alipotembelea mabanda mbalimbali kama likiwamo la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) pamoja na la UDSM, akisema biashara ni kuonesha kile kinachozalishwa na nchi husika, ili kijipatia soko.

“Upo umuhimu wa kukitangaza unachokizalisha hivyo
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ni fursa kwa Watanzania, ili kutangaza kilichopo nchini hasa sekta ya biashara kwa kile tunachokitengeza nchini.

“Unapotengeneza bidhaa kama batiki au sabuni vitaonekanapale utakapotangaza.
Wapo wafanyabiashara wa ndani wanaofanya biashara, ila wapo wa nje watakuja kuonesha ya kwao wanachokifanya kwa kuonesha kile wanachoweza kuwekeza,” amesema Kikwete.

Amesema kile wanachokija kukiangalia wageni, kunahitajika zaidi nchini na kwenda kukizalisha kwa wingi wanaporudi nvmchi mwao pamoja na kufahamu aina ya bidhaa inayohitajika na kutaka kuwekezwa.