
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Manyara.
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CHama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Hanang mkoani Manyara kutoa ushirikiano kwa Serikali ili iendelee kuwaletea maendeleo.
Pia, amewataka kuendele kulinda na kudumisha umoja, amani na mshikamano katika maeneo yao, akisema kuwa bila amani hakuna maendeleo yatakayofanyika.

Hayo ameyasema leo Juni mosi, 2026 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi alipotembelea Shina Namba moja, Kata ya Masakta, Tawi la Masakta lililopo katika Wilaya ya Hanang.
“Tumekusanyika hapa kwa sababu kuna amani, bila amani pengine tusingekuwepo hapa na shughuli zisingefanyika, hivyo niwaombe mlinde nyumbani kwenu msikubali wageni waje wawaharibie.
Lakini pia, endelee kutoa ushirikiano kwa Serikali ili iendelee kuwafanyia makubwa. Lakini pia vongozi tutambue kuwa nafasi zetu tulizonazo ni kwa sababu ya CCM na bila CCM kusingekuwa na mbunge, mwenezi, mwenyekiti nk hivyo kila mmoja aheshimu nafasi aliyopewa na chama.
Aidha, Kihongosi amewaahidi wakazi wa eneo la Maskata kufuatilia suala la kupandisha hadhi Zahanati yao na kuwa Kituo cha Afya, kwani ina miaka 20 sasa ikiwahudumia huku idadi ya watu ikiongezeka.

Akisoma taarifa kwa Mwenezi huyo wa CCM, Mwenywkiti wa Shina namba moja, Dismas Gwasma, amesema wanaomba zahanati hiyo ipandishwe hadi ili waweze kupata huduma za madaktari, huduma za mama na mtoto, upasuaji pamoja na nyumba za madaktari.
Gwasma amesema, Shina namba moja, Tawi la Masakta, lina idadi ya wanachama 45 ambao wamesajiliwa kwenye mfumo wa kielektroniki.
Leo Juni mosi, Kihongosi ameanza rasmi ziara yake katika mkoa wa Manyara, ambapo atatembelea na kukagua miradi ya maendeleo, kuangalia uhai wa chama pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi kupitia mkutano wa hadhara.



More Stories
DC,Chirukile ziarani Kongo kujenga mahusiano ya Kidiplomasia,uchumi
NMB yaiweka Tanzania kwenye ramani ya Mitaji Cambridge
SKA yahamasisha waandishi wa habari kuwania Tuzo