May 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kibweta Cha Mwalimu Nyerere kina mchango mkubwa kwenye uzalendo na maadili MNMA

Na Rose Itono,Timesmajira

CHUO Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimesema kinamchango mkubwa wa kukuza uzalendo na maadili kwa maendelea endelevu kupitia uanzishwaji wa Kibweta

Akizungumza kwenye kusanyiko la wahitimu wote waliomaliza chuoni hapo Dar es Salaam jana mchokoza mada ambaye ni Mhadhiri chuoni hapo Dkt Ahmad Sovu amesema kazi ya Chuo kikuu chochote duniani ni kufundisha, kufanya tafiti za kitaalamu zinazotatua changamoto na kutoa ushauri wa kitaalamu

Amesema Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kina mchango mkubwa wa katika kukuza uzalendo na maadili kwa maendelea endelevu

‘ Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza uzalendo na maadili kupitia kitengo maalumu Cha Kibweta kilichoanzishwa kwa ajili ya masuala hayo,’amesema
Dkt Sovu

Ameongeza kuwa kupitia Kibweta Cha Mwalimu ambacho ni kitengo maalumu kwa ajili ya masuala ya maadili Kuna kazi kubwa ya kuilunda thamani kuenzi na kuyaendeleza mambo yaliyokuwa yakifanywa na Mwalimu Nyerere katika katika uzalendo uzalendo na maadili ya taifa.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo walioshiriki muhadhara chuoni Kivukoni Dar es Salaam Jana

Mmoja kati ya wachangiaji wa kusanyiko hilo ambaye alikuwa ni Rais wa Serikali ya wanafunzi naka 2018/19 Gedfrey Malila alisema Ili tuenzi sifa nzuri ya maadili tuliyojifynza vijana wanapaswa kuacha tabia ya uongo.

Ameongeza kuwaasa vijana kutotumia usomi kama njia ya kujinufaisha badala yake aliwataka kuwa wakweli kama ilivyokuwa enzi za wazee wetu waliopita

Ameongeza wazee wa zamani kwa kusema walikuwa na uzalendo wa kweli tofauti na Sasa ambapo kundi kubwa la vijana limekuwa likijificha kwa kujifanya wazalendo huku wakiwa na uongo uliokithiri

Naye Katibu wa kusanyiko hilo Jumanne Muruga amewataka wanafunzi kukutangaza vema Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuwa na uzalendo na maadili

Amesema ni wazi kuwa taifa linajisifia viongozi Bora waliopita chuoni hapa kwani wamekuwa ni mfano wa kuigwa wakati wakitejeleza majukumu Yao ya kazi kwa maendelea endelevu ya taifa hili.