January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kessy atua Mtibwa Sugar

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

TIMU ya Mtibwa Sugar imekamilisha usajili wa beki wa kulia Hassan Ramadhan Kessy akitokea Nkana Red Devils ya Zambia.

Huo ni usajili wa tano wa ndani ya Mtibwa msimu ambao wanaboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu 2020/2021 baada ya msimu uliomalizi kutokuwa mzuri kwao.

Mtibwa ilifanikiwa kujinusuru kushuka daraja baada ya kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting na kumaliza msimu wakiwa nafasi ya 14.