May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu CWT awaasa wanafunzi chuo kikuu Dodoma

Na Joyce Kasiki,TimesMajira OnlineDodoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha walimu (CWT) Mwalimu Deus Seif amewaasa wanafunzi wa kada ya ualimu katika chuo kikuu cha Dodoma wanaotarajia kuhitimu masomo yao mwaka huu kuitumia benki ya Mwalimu (MCB) kwani imeanzishwa kwa ajili ya kuwakomboa walimu.

Akizungumza katika kongamano la wanachama wa chama cha walimu katika chuo hicho (UDOSTA) la kuwaaga wanachama wa mwaka wa tatu,Seif alisema,walimu wanapaswa kuitumia benki hiyo kwani ya kwao na imefunguliwa ili kuwakomvoa walimu dhidi ya changamoto nyingi zinaowakabili walimu nchini .

Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu (CWT), Mwalimu Deus Seif akizungumza na wanachama wa UDOSTA (hawapo pichani) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Hata hivyo Katibu Mkuu hiyo amesema,inashangaza kuona idadi kubwa ya walimu bado hawataki kuitumia benki hiyo na badala yake wamekuwa wakitumia benki nyingine na kuzinufisha huku ya kwao ikibaki inasua sua.

“Hapa ndipo walimu tunashangaza ,wakati watu wa Ulaya wanauliza tumewezaje chama cha wafanyakazi kufungua benki ,lakini benki sisi wenyewe hatuitumii,

” Mwaka 2018 waliokuwa wakiitumia MCB walikuwa ni walimu 3,000 tu ,yaani ni kama mtu una mgahawa wako halafu unaenda kula mgahawa wa jirani,

“Naomba tuamke walimu wenzangu tutumie benki yetu ,lakini pia mnapaswa kujua hii ni vita ya kiuchumi hata wenye mabenki wanajua kwamba walimu wote wakisema watumia MCB benki zao zinaweza kufisilika.” amesema Seif.

Kufuatia hali hiyo amesema CWT kimeshatoa maelekezo kwa viongozi wote kuhakikisha malipo yote kutoka CWT yanapitia MCB

Katika hatua nyingine amewaasa wanachama hao hususan waliopo kazini kuhakikisha wanatoa maoni kuhusiana na ianzishwaji na bodi ya kitaaluma ya walimu .

“Sheria ilishatungwa lakini hatujakubaliana nayo kwani bodies hiyo haimnufaishi mwalimu na badala yake imekuwa kandamizi,kwenye sherehe ya wafanyakazi mwaka huu tulimwomba Rais Samia Suluhu Hassan naye amekubali omvi letu na sheria hiyo inarudishwa kwetu,nawasihi tutoe maoni yetu kikamilifu.

” Amesisitiza na kuongeza kuwa

“Hii sheria ni yetu sisi walimu,na sisi ndio tunaojua changamoto zinazotukabili,tutoe maoni yetu,siyo maoni yatolewe na taasisi yoyote ile.

Akizungumza katika kongamano hilo mwakilishi kutoka MCB John Mhina amesema benki hiyo inatoza TIBA mdogo tofauti na benki nyingine lakini pia huduma mbalimbali ikiwemo ya mikopo,tukutane Januari ,Mwalimu jikimu na huduma nyingine nyingi zinaoweza kumkomboa mwalimu.

“Kwa mfano huduma hii ya tukutane Januari,tuliianzisha baada ya kuona mwezi Januari una changamoto nyingi ,tukasema mwalimu anaweza kuwekeza fedha zake katika huduma hii NA kuzitoa mwezi januri na kufanya mambo muhimu ikiwemo ulipaji wa ada za wanafunzi.alisema.

Pia amesema hufuma mikopo inamwezeaha mwalimu pamoja na walimu wastaafu kuepukana na mikopo umiza ambayo imepelekea walimu wengi kufislika na kubaki masikini.