January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu CCM athibitisha kupokea barua ya Spika Ndugai kujiuzulu

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BAADA ya Masaa kadhaa kupita tangu Spika wa Bunge Job Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amethibitisha kupokea barua ya Spika huyo Ndugai ya kujiuzuru nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu Chongolo ameeleza kuwa mchakato wa kumpata Spika mwingine baada ya nafasi hiyo kubaki wazi unaendelea.