January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kanisa Halisi la Mungu lasherehekea majira mapya ya mwaka mpya ya kanisa

Na David John, TimesMajira Online

KANISA halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta Namanga Kinondoni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Januari nne limesherekea majira mapya ya mwaka mpya ya kanisa hilo huku Mchungaji wa kanisa Baba halisi akiwataka waumini wake na watanzania kwa ujumla kurejea katika majira wakati na kabla ya uharibifu. .

Akizungumza katika ibada maalumu ya majira mpya ya kanisa hilo ambayo imekwenda sambamba na uzinduzi wa kalenda ya majira mapya ambayo imefanyika kanisani hapo Baba halisi amesema kuwa niwakati sahihi watu kusahau mabaya waliyotendewa na badala yake wametakiwa kuishi Kama moyo upendavyo.

Amesema kuwa ibada hiyo imeshirikisha vituo mbalimbali vya kanisa halisi la Mungu Bab, kutoka ndani ya Tanzania na nje ambapo kupitia ibada hiyo yalifanyika maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea rais Samia Suluhu Hassan pamoja na familia yake ili aendelee kuliongoza taifa kwa amani na usalama.

Baba halisi amesema kuwa lazima kumuombea kiongozi mkuu wa nchi kwani kupitia yeye taifa liko salama na watu wake wana amani nakwamba ujumbe wa ibada hiyo ni ”Ramani mpya Jengo jipya na Maisha Mapya yaliyowaingiza katika Majira yasiyo na Uharibifu. ”

Baba halisi ameongeza kuwa waumini wanatakiwa kujua kuwa kanisa ni moyo ulioumba kila kitu hivyo watu wakiulizwa wasipapase katika kutoa majibu yake nakwamba kanisa au taasisi kila iliyoumbwa na kujitegemea katika safu iliyokusudiwa.

” Magonjwa yamilipuko, ukame. Umasikini, ufukala vinapokutana na kanisa vinakaa kimya na kutakiwa kunyamaza kabisa. Kwamaana havina nafasi kabisa. “Amesema Baba Halisi

Nakuongeza kuwa ” majira halisi ndio chanzo chema na apatae Kanisa amepata chanzo halisi nakuwa nivema wanadamu kumwabudu aliyeumba. “amesema

Amefafanua kuwa Chanzo halisi anakaa ndani ya moyo wake,lakini jambo muhimu nikutenda kwa haki..

Wakati huohuo Baba halisi amemsifu Spika wa Bunge la Tanzania Kwa kitendo chake cha kujitokeza hadharani kuomba msamaha nakwamba kitendo hicho kinadhihirisha kwamba nchi iko Salama.

Alisema kuwa hatua ya kutubu hadharani kiongozi mkubwa Kama yeye niwazi kuwataifa la Tanzania ni la chanzo halisi ” taifa hili linapendwa na Chanzo halisi ndio maana tuna amani na ndio maana unaona kiongozi mkubwa Kama huyu anaomba radhi.”alisema Baba Halisi.

Nakuongeza Kuwa ” yeye amestajaabu sana hasa kuona kiongozi mkubwa Kama huyo anatubu mbele ya taifa. ameshangaa Sana nakuamini kwamba taifa la Tanzania limebarikiwa.