November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KAMPUNI ya Oryx Gas yajitosa kivingine kumuunga mkono Rais Samia



Na Penina Malundo, Timesmajira

KAMPUNI ya Oryx Gas imesisitiza kuendelea kuunga mkono kwa vitendo dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha ndoto yake ya kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2032

Katika kuunga mkono jitihada hizo Kampuni hiyo imekabidhi mtungi wa gesi wenye kilo 15 ukiwa na jiko lenye plate mbili kwa wahariri na waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha kwa vitendo kampeni hiyo ya Rais Samia ili jamii ione haja ya kutumia ishati safi ya kupikia.

Hayo yalisemwa Leo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx, Benoite Araman, wakati akizungumza na wahahariri na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa umuhimu mkubwa kampuni hiyo imeamua kukutana na kundi la wanahabari ambalo linaushawishi mkubwa, ambao utasaidia kuhamasisha kwa vitendo utumiaji wa nishati hiyo safi ya kupikia.

“Rais Dkt. Samia ameeleza dhamira ya kuona  asilimia 80 ya Watanzania inatumia nishati safi ya kupikia, Oryx Gas tumedhamiria kwa vitendo kufanikisha ndoto ya Rais wetu,”amesema na kuongeza;

“Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na Mama Lishe, watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali na leo tunafurahi kukutana nanyi wahariri na waandishi wa habari katika tukio hili la kuwakabidhi mtungi wa gesi wenye kilo 15 ukiwa na jiko lenye plate mbili”amesema.

Amesema  vyombo vya habari vimekuwa vikishiriki katika matukio mbalimbali yanayohusu Oryx hasa katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi, hivyo kwa ushirikiano wa vyombo hivyo vya habari ni ishara ya kurudisha shukrani zao kwa vyombo hivyo.

Araman, amesema kupitia mkutano huo, umewawezesha kufungua mlango wa kuhamasisha waandishi wa habari kote nchini kutumia nishati safi na hatimaye kufikia lengo la Rais Dk Samia.

”Oryx Gas Tanzania mpaka sasa tumeshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 maeneo mbalimbali nchini na kiasi cha bilioni 1.5 kimeshatumika,”amesema na kuongeza

“Tunaahidi kama ambavyo tumekuwa tukiahidi siku zote tutaendelea na kampeni hiyo kadri ya uwezo wetu, kuna faida nyingi za kutumia nishati safi ikiwemo kwa kutumia gesi ya Oryx kwenye taasisi mbalimbali ambayo inasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi husika kutafuta nishati nyingine kama kuni na mkaa,”amesema Araman.

Araman amesema faida nyingi ya utumiaji wa gesi safi ya kupikia kwa kutumia Oryx Gas ni kulinda mazingira kwa kutokomeza ukataji wa miti, kwani misitu ni muhimu kwa kudumisha viumbe hai, kuhifadhi udongo, kusaidia mizunguko wa maji na pia uharibifu wa misitu .

Mbali na faida hizo pia inasaidia kulinda afya ya wanawake ambao wanaathirika kwa moshi inayotokana na mkaa na kuni,inaepusha akina mama na watoto kuumia kwa kubeba kuni nzito na kuepuka kujeruiwa na wanyama wakali wakiwa wanatafuta kuni