Na Iddy Lugendo,timesmajira,Online
KAMPUNI ya IStore inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa ya ‘Apple’ imetangaza kuzindua kundi maalumu la watu ambao wanatumia bidhaa hizo nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa IStore kundi hilo litawawezesha watumiaji wa bidhaa za ‘Apple’ kukutana na kutengeneza urafiki na watumiaji wengine wa bidhaa hizo pamoja na kuuliza maswali na kupata majibu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu bidhaa hizo.
Wakizungumza na TimesMajira juzi, wamiliki wa IStore wamesema kundi hilo litajumuisha watu wa rika zote, wenye uelewa wa kati kuhusu kompyuta, wataalamu wa kompyuta na wengine kutoka katika fani na taaluma mbalimbali.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa bidhaa za ‘apple’ nchini Tanzania haswa simu za I phone na kupelekea kutanuka kwa matumizi ya bidhaa hizo hapa nchini
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote