November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni Dnata imetangaza uwekezaji katika sekta ya usafiri wa anga Zanzibar.

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni inayotoa huduma za usafiri wa anga duniani, imetia saini mkataba wa makubaliano na Serikali ya Zanzibar, pamoja naShirika la ndege la Emirates na SEGAP, katika ukarabati ya wa miundombinu ya viwanja vya ndege na wataalamu wa uendeshaji kutoka Egis, na meneja wa hazina ya hisa za kibinafsi AIIM.

Ushirikiano huo, dnata itasimamia shughuli zote za Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (ZNZ) kilichojengwa hivi karibuni cha (T3), huku SEGAP ikisaidia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) katika usimamizi. Emirates Leisure Retail itashirikiana na MMI kama mfanyabiashara mkuu wa vyakula na vinywaji vyote katika maduka kibiashara ya ndani na biashara za kimataifa.

dnata itatoa huduma za ubora wa uwanja wa ndege na kutoa kuhuduma kwa abiria, mashirika ya ndege ZNZ, kuhakikisha uendeshaji wa safari za ndege unakuwa salama wa uhakika na kwa bora wa hali ya juu. dnata inatarajia kushughulikia safari Zaidi ya 4,000 kwa mwaka katika uwanja wa Amani Abeid Karume.

dnata pia kuwekeza Zaidi katika kituo cha kisasa cha mizigo katika uwanja huo huku ikinzisha huduma za mizigo na, kusaidia biashara ya ndani ya uwanja wa ndege. Kituo hicho kitazingatia viwango vya hali ya juu ya tasnia ya usafirishaji na upokeaji mizigo kutoka sehemu mbalimbali na kuhakikisha mizigo iyo inatunzwa kwa usalama, utunzaji huo utazingatia zaidi katika bidhaa zinazoharibika, dawa, bidhaa hatari, wanyama hai, injini za ndege na magari.

Kwa kuongezea, dnata inazindua huduma za meet & greet yaani Kukutana na kusalimiana kupitia chapa yake ya kutoa huduma inayojulikana kama marhaba katika viwanja wa ndege na abiria kufurahia safari wakati akiwa katika uwanja wa ndege wakati wa kuingia ndani ya ndege hadi wakati wa kushuka katika uwanja wa ndege.

dnata kwa Tanzania ni mwekezaji wa kwanza mpaka sasa inatoa huduma bora na salama kwa utunzaji wa mizogo, upishi na usafiri katika nchi 36.

Steve Allen, Makamu wa Rais Mtendaji wa dnata na Mwenyekiti wa Emirates Leisure Retail na MMI, alisema: “Tunafuraha ya kupanua wigo wetu barani Afrika na kuanzisha shughuli katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Tunaimani kwamba uwekezaji wetu katika sekta ya anga utachochea utalii na biashara na kuleta manufaa makubwa kwa wafanyabiashara wa Zanzibar na jamii kwa ujumla.

“Shauku yetu ni kutoa huduma kwa ubora na ushirikiano mkubwa kulingana na uzoefu wetu kufanya kazi kimataifa katika utunzaji wa uwanja wa ndege, ukarimu abiria akiwa uwanja ndege na huduma za F&B zitakazohakikisha ubora thabiti katika kila hatua ya safari abiria akiwa uwanjani. Bunifu mbalimbali zitaoneshwa katika uwanja wa ndege ambapo itatoa uzoefu jumuishi kwa abiria huku tukionesha mila na mtindo ya wakazi wa Zanzibar.

“Tunatarajia ushirikiano wenye tija na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na SEGAP.”

Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi alisema: “Kuzinduliwa kwa jengo letu jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ni hatua ya mabadiliko katika juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa kisiwa kinachotambulika duniani kwa utalii na biashara. Ushirikiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na dnata unathibitisha dhamira yetu ya ubora wa kimataifa katika kutoa uzoefu usio na wasiwasi kwa wageni wote wa kimataifa. Tunatazamia kupanua wigo wetu wa kimataifa katika kuwezesha biashara na uwekezaji kupitia uwezo wetu wa kushughulikia usafirishaji wa abiria na ndege.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mauzo wa Egis, Christian Laugier alitoa maoni; ” Tunatoa heshima kuleta utaalam wetu katika ukuzaji wa uwanja wa ndege, utendakazi na matengenezo kwenye mradi. Timu yetu itazingatia utendakazi katika maeneo yote, ikiwa ni pamoja na miundombinu, uendeshaji, usalama, utawala na fedha. Juhudi zetu zitakuwa katika kufanya uwanja wa ndege na usafiri wa anga kuwa vichocheo bora zaidi vya ukuaji wa utalii katika eneo ambalo lina kila kitu cha kuvutia wageni wanaoingia Zanzibar, Hii ni hatua muhimu ambayo inafungua ushirikiano na Zanzibar, ambapo tumejiandaa kufikiria uwekezaji zaidi katika uendelezaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege.”