January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

kampeni ya natembea na mama, kumuunga mkono Rais Samia yazinduliwa

Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online

KATIKA kuendeleza jihada za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kijana wa kitanzania anayehamashisha uzalendo kwa Taifa Ikuzi kicheko maarufu kama Mzalendo halisi amezindua rasmi kampeni ya Watanzania kumuunga mkono Rais Samia.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mzalendo amesema Kampeni hiyo itaanzia Kilwa na kuelekea visiwani Zanzibar oktoba 29.

“Tunaanzia katika Ufukwe wa Ununio tukitembea kwa kutumia usafiri wetu mpaka Zanzibar katika kampeni ya natembea na Mama”. Amesema Mzalendo Halisi

Amesema kwenye kampeni ya Natembea na Mama watembe kwa Mguu katika miundo Mbinu yote inayopatikana na katika visiwani Zanzibar ikiwemo mashule Hospitali katika kumsapoti Rais Samia.

Aidha amewataka Watanzania ambao watapenda kushiriki katika kampeni hii kwa kutoa fedha tasilimu ama kitu chochote ambacho kitaweza kusaidia kupeleka katika miradi mbalimbali ambayo watembelea katika visiwa vya Zanzibar.