Mshindi wa promosheni ya maokoto ndani ya kizibo mzunguko wa nane Mrashan Kilabila(kulia) akipokea mfano wa hundi yake kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Desdelius Method, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye bar ya Mwanza live.
Mshindi wa shindano la Maokoto kutoka Wilaya Kilosa linaloendeshwa kupitia vinywaji vya kampuni ya bia ya Serengeti SBL , Maimuna Ally (kushoto) akipokea hundi ya mfano ya TSh 500,000 kutoka kwa Mwakilishi wa mauzo wa kampuni ya SBL Shomari Mohammed, hafla ya kukabidhi zawadi hiyo imefanyika Dumila Bar iliopo Dumila wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Mshindi wa promosheni ya maokoto ndani ya kizibo mkoani Tabora Godfrey Mwakasyuka(kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Masoko wa Serengeti Breweries Limited mkoa wa Tabora Azaria Mbughuni, wakati wa hafla ya makabidhiano kwenye bar ya Serengeti.
Meneja wa Savoy Bar Given Micheal(kulia) akitoa neno la shukrani wakati akipokea hundi ya shilingi laki tano kwa niaba ya mmoja wa washindi wa droo ya nane ya Serenegetu Maokoto ndani ya kizibo Karisto Alfred kutoka kwa Balozin wa kampeni hilo Bill Nas (kushoto) wikiendi hii Buza, Dar es salaam.
Mshindi wa shindano la maokoto kutoka Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro linaloendeshwa kupitia vizibo vya vinywaji vya kampuni ya bia ya serengeti SBL, Fatuma Sudi (Kulia) akipokea hundi ya mfano ya Tsh 500,000 kutoka kwa Godwin Urasa ambaye ni Mwakilishi wa mauzo ya kampuni ya SBL Wilaya ya Hai na Siha kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hiyo ilifanyika Msami Bar iliyopo Mji mdogo wa Bomang’ombe Wilayani Hai.
Mmoja wa washindi wa Sefrengeti Ndani ya Kizibo Beatrice Mwazembe (kulia) akipokea hundi ya shilingi laki tano kutoka kwa mwakilishi wa Serengeti Breweries Limited Doreen Tagalile wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi fedha hizo eneo la Buza jijini Dar es salaam wikiendi hii.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto