Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa.
katika mazungumzo hayo walijadili namna ya kuboresha uhusiano wa TRA na TPA na kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kwa karibu zaidi ili kuimarisha utendaji kazi kwa taasisi zote mbili.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 31.07.2024 katika ofisi Kuu za TPA jijini Dar es Salaam.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam