Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa.
katika mazungumzo hayo walijadili namna ya kuboresha uhusiano wa TRA na TPA na kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kwa karibu zaidi ili kuimarisha utendaji kazi kwa taasisi zote mbili.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 31.07.2024 katika ofisi Kuu za TPA jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda (wa kwanz akushoto) akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa (Kulia) wakijadili namna ya kuboresha uhusiano wa TRA na TPA na kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kwa karibu zaidi ili kuimarisha utendaji kazi kwa taasisi zote mbili. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 31.07.2024 leo katika ofisi Kuu za TPA jijini Dar es Salaam.Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda akisalimiana na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile walipokutana katika kikao kati ya Kamishna Mkuu wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa kilichofanyika leo katika Ofisi za TPA, jijini Dar es Salaam.
More Stories
Watendaji Ubungo wapongeza ubunifu ununuzi wa mitambo
Madaktari bingwa kutoa huduma ya kinywa Arusha
Mixx, Hub wakusanya maelfu fainali kombe la dunia Zanzibar