November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya Siasa Shinyanga yawapongeza wananchi Msalala kwa kuunga juhudi za serikali

Na Patrick Mabula,TimesMajira Online Kahama

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Shinyanga imewapongeza wananchi wa halmashauri ya Msalala , wilayani hapo kwa moyo wao wa kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la maendeleo na kuweza kukamilisha zahanati 18 na vituo vya afya 7.

Pongezi hizo zimetolewa na kamati hiyo wakati ilipotembelea kuona utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika miradi ya maendeleo kwa fedha za serikali na nguvu za wananchi wa Msalala.

Akiwa ameongoza kamati hiyo Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga,Mabala Mrolwa akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa huo Christina Mdeme na kamati ya ulinzi na usalama waliweza kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo afya, elimu na miundombinu ya barabara.

Akiongea kwa nyakati tofauti tofauti katika miradi hiyo Mwenyekiti huyo , Mrolwa aliwapongeza viongozi na wananchi wa Halmashauri ya Msalala kwa kutekeleza vizuri miradi ya maendeleo na kuweza kukamilisha zahati 18 kila kata na vituo vya afya 7.

Awali wakitoa taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji katika mirad hiyo iliyotembelewa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala , Charles Fussi wamesema fedha zilizotolewa na Serikali pamoja na pesa za mapato ya ndani wananchi waliunga mkono kwa nguvu zao kwa kujenga maboma na kuweza kukamilsha miradi hiyo ikiwemo ya elimu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Christina Mdeme akiongea katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Msalala uliofanyika katika Kata ya Segese amesema Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan , imeweza kutoa zaidi ya bilioni 1.1 kwa Msalala katika miradi ya maendeleo.

Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Busangi , Evamary Elias alipokuwa akitoa taarifa ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ntundu amesema wananchi walitumia nguvu zao na kukamilisha boma na Serikali ikatoa kiasi cha milioni 63.5 kukamilisha majengo yote kwa gharama ya milioni 52.9 na pesa iliyobaki wanatarajia kununua vifaa tiba.

Kwa upande wao wananchi wa Msalala wameipongeza serikali ya Rais Dkt .Samia na kuomba wapatiwe watumishi katika zahanati 18 walizokamilisha kwa kila kata na vituo vya afya 7 pamoja na vifaa tiba kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa kwenye kada ya sekta hiyo.

Mbunge wa Jimbo mbo la Msalala , Idd Kassim aliipongeza serikali kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo kwa jimbo lake kiasi cha zaidi ya bilioni 1.1pamoja na wafadhili mbalimbali wa maendeleo na kuwaahidi wananchi kuwa ataendelea kushirikiana nao katika suala la kuhakikisha wanapata maendeleo wanayoyatarajia .

Wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM ya mkoa wa Shinyanga wakichenza ngoma na Sungusungu wa kijiji cha Tundu kata ya Busagi halmashauri ya Msalala baada ya kukagua ukamilishaji wa Zahanati yao walipokuwa walipokuwa wakitembelea kuona utekelezaji wa irani ya CCM.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Christina Mdeme akiwa amemunyayua mkono Mbunge wa jimbo la Msalala , Idd Kassim kumpongeza na wananchi wa Msalala kwa kukamilisha zahanati 18 kila kata na vituo vya afya 8 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Segese , Halamshauri ya Msalala , wilaya ya Kahama alipokuwa na kamati ya siasa ya CCM ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kutembelea miradi na kuona utekelezaji wa ilani ya chama.