Raphael Okello, Timesmajira Online,Mwanza
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi ,uboreshaji na upanuzi wa bandari ya Mwanza Kaskazini iliyopo jijini hapa.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya bilioni18.6 unatarajiwa kuchukua miezi 18 kukamilika. ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 30 .
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Suleiman Kakoso wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo ambapo ameeleza pia wameridhishwa na utekelezwaji wa miradi mingine ya TPA walioitembelea.
Kakoso amemtaka Meneja wa bandari za Ziwa Victoria kuendelea kusimamia mradi huo na kumalizika kwa wakati ili ilete faida kwa watanzania wote.
Meneja wa bandari za Ziwa Victoria Erasto Lugenge,ameahidi kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kukamilisha kazi kwa wakati kuendana na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika eneo hilo.
Mapema mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Amos Makala ameeleza kuwa upanuzi na uboreshwaji wa bandari uendane na dhamira ya ubinafsishaji wa bandari ya Dar es Salaam uliofanywa hivi karibuni.
Ambapo kutokana na ahadi ya kukamilika kwa ujenzi wa meli ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” unaotarajiwa kukamilika Mei mwaka huu inahitajika juhudi za haraka kukamilisha upanuzi wa ghati katika bandari hiyo.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi