*Ni kuweka uwazi na uwajibikaji wa mikataba
*Lengo ni kuhakikisha hakuna nafasi ya kuingia mikataba mibovu
Judith Ferdinand, Timesmajira Online
Mkurugenzi wa kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi(PPPC),David Kafulila,amesema kila hatua ya kuchakatwa mikataba ya ubia(PPP), ni hatua ya uwazi na uwajibikaji huku akisisitiza kuwa mikataba ikiwa mibovu haiwezi kuleta tija kwenye uwekezaji.
Kafulila amebainisha hayo wakati akizungumza katika moja ya kipindi cha kituo cha runinga,nchini hapa,ambapo amesema kutokana na mikataba mibovu, Serikali ilianzisha kituo hicho cha Ubia,ili uwekezaji uweze kuleta tija.
“Pengine Serikali sasa kutokana na uzoefu wa mikataba mibovu ikatengeneza na kukazia sheria kwa kuanzisha kituo cha Ubia, kwa lengo la kuhakikisha mchakato mzima wa mikataba unakuwa na uwazi na uwajibikaji na inapita kwenye macho mengi na hakuna nafasi ya kuingia mkataba mibovu,”amesema Kafulila.
Amesema mikataba inaanzia kwa mamlaka husika kuchakatwa akitolea mfano kama ni TANESCO na Wizara yake ya Nishati, akitoka pale utaenda kwenye kituo cha ubia ambacho kitaangalia namna gani wanaunda ule mkataba na hatua zote za kuchakata ule mkataba.
“Lakini baada ya kituo cha Ubia kuna mamlaka inayopitisha pale juu inaitwa Bodi ya Masuala ya Ubia,ambayo yenyewe inaundwa na Makatibu wakuu na kamishina wa TRA, Mkurugenzi wa sasa wa Uwekezaji na sekretarieti yake ni kituo cha Ubia.Mfumo huo uliwekwa hivyo ili kuongeza uwazi na uwajibikaji kwenye kuchakata hiyo mikataba,”.

More Stories
Senyamule:Serikali inapaswa kuzitambua Kampuni zinazofanya biashara ya ardhi
Serikali kuendelea kupanua fursa elimu Singida
Kumekucha CDF Cup 2026, NMB yaweka Sh milioni 150