Na David John, timesmajira, online
KADA wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya kipawa wilayani ilala mkoani Dar es Salaam Mabindo Ngulu amechukuwa fomu ya udiwani wa kata hiyo baada ya kujipima na kuona anauwezo wa kuwaongoza wanakipawa.
Ngulu amesema kuwa kata ya kipawa imekuwa mikononi mwa upinzani na kusababisha kudorola kwa Maendeleo hivyo kutokana na hali hiyo ameshawishika kuchukua fomu ili kuweza kuwania nafasi ya kuwa Diwani wa Kata hiyo.
Akizungumza na Times Majira leo baada ya kuchukuwa fomu amesema kuwa amesukumwa kufanya hivyo kutokana na kata hiyo kukosa kiongozi sahihi ngazi ya kata na kuweza kuwatumikia wananchi wa kata ya kipawa.
“Leo kama mnavyoona ndungu zangu wanahabari nimejitosa kuchukua fomu hii kwa nia moja tu ya kupata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa kata yangu ya kipawa.”amesema na kuongeza
“Sasa hivi ni muda wa kuchukua fomu tu na kwenda kuijaza na baadae narudisha, michakato ndani ya chama itakapokamilika na hatimaye jina langu kurudi hapo sasa nitasema mipango yangu zaidi ,”amesema
Akizungumzia uzoefu wake kwenye siasa amesema yupo kwenye siasa kwa miaka mingi na Kama ilivyoada kwa wanasiasa hata yeye ameshapita vyama vingine huko nyuma lakini sasa yuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM na alishawahi kugombea nafasi kadhaa.
Pia amesema kutoka na utaalamu wake wa kuchanganua vitu anaamini anauwezo mkubwa wa kufanya jambo endapo Chama chake kitampa ridhaa na kupitishwa kuwa mgombea udiwani kwenye kata hiyo
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa