LEO ni siku ya kihistoria, Siku ambayo vizazi vijavyo vitaisoma vitabuni. Siku ambayo Tanzania imeamua kujitegemea kweli kweli.
Pongezi kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa ujasiri wa kuamua na kutekeleza mradi huu mkubwa uliohitaji maamuzi magumu sana ili kufanikiwa sambamba na kumpongeza kila mtanzania aliyetoa nguvu, jasho na akili yake ili mradi huu ufanikiwe.
HISTORIA YA NDOTO – KUTOKA NYERERE HADI LEO
Ili tuelewe ukubwa wa leo, turudi nyuma.1967: Azimio la Arusha Hayati Mwalimu Nyerere alisema “Bila viwanda, bila umeme, bila kilimo cha kisasa – Uhuru wetu hautakuwa na maana”. Aliona tatizo la nishati miaka 60 iliyopita.
Changamoto za Miaka 60 Tulijaribu miradi midogo midogo. Tulitegemea mvua. Tulitegemea mafuta ya gharama kubwa, matokeo yake viwanda vilifungwa, vijana wakakosa ajira.
2021: Kazi Iendelee
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, swali lake lilikuwa moja:
“Tutatatuaje tatizo la msingi la nishati?” Jibu likawa: Twende kwenye chanzo, Twende kwenye maji yetu. Twende kwenye mradi mkubwa”.
Leo tunashuhudia mtego wa umaskini ukikatika. Huu ni mwendelezo wa maono ya uongozi chini ya Dkt Samia si mradi wa mtu mmoja.
Bwawa hili lina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kuangazia nchi nzima mara mbili. Lina hifadhi ya maji ya kutosha kulima hekari milioni. Lina dhamira moja kutoa umeme wa bei nafuu wa uhakika, kwa miaka 100 ijayo.
FAIDA 5 KUBWA KWA UCHUMI WA TAIFA.
Hii ndiyo injini mpya kwa taifa la Tanzania ikiwa na faida kubwa kadhaa zikiwemo:
1. Mapinduzi ya Viwanda – “Tanzania Yetengeneze”
Kwa sasa gharama ya umeme ni asilimia 40 ya gharama ya uzalishaji. Ikishuka, kiwanda cha nguo Arusha kitashindana na cha China. Mfano: Kiwanda kimoja cha kati kinatoa ajira 500. Tukipata viwanda 1000, tunatoa ajira milioni 1/2.
2. Kilimo cha Umwagiliaji na Usalama wa Chakula
Tuna ardhi ya hekari milioni 44 zinazoweza kulimwa. Tumekuwa tunatumia hekari milioni 10 tu kwa sababu ya mvua. Sasa kwa maji + umeme, tutalima mara 3 zaidi. Matokeo: Tutaacha kuagiza sukari, mafuta ya kupikia, mchele na kwa uhakika tutaweza kuuza nje ya nchi na Taifa likiwa na uhakika wa kujitegemea na chakula.
3. Madini na Thamani Ongezwa
Madini yetu ya dhahabu, nikeli, graphite yanahitaji umeme mwingi kuyeyusha. Sasa tutayeyusha hapa Tanzania, si nje. Matokeo: Badala ya kuuza tani ya madini kwa $2000, tutauza bidhaa iliyotengenezwa kwa $50,000.
4. Utalii na Uchumi wa Usiku
Miji yetu itakuwa na taa masaa 24. Watalii watakuja, wafanyabiashara watakuwa na ujasiri wa kufungua biashara zao ambapo Uchumi utakuwa wa saa 24 na shauku ya vijana kujituma kwenye sekta ya utalii itaongezeka na kuifanya kuwa mkombozi katika soko la ajira nchini.
5. Kuokoa na Kujenga
Tunapata faida ya kuokoa dola milioni 400 kwa mwaka. Hiyo fedha inajenga vyuo 20, hospitali 50, na barabara 1000km kila mwaka Taifa litatoka kwenye utegemezi wa misaada hasa ya kibajeti jambo ambalo ni heshima kubwa kwa Tanzania yetu mbele ya macho ya dunia.

FAIDA KWA MTU WA KAWAIDA Maendeleo bila kugusa kaya hayana maana na yatachelewa kutafsirika kwenye dhana ya maendeleo chanya.
Mama wa Soko: Atapata friji. Mboga zake hazitaharibika tena kwa kukosa umeme wa uhakika lakini atakuwa na fursa ya kuuza katika nyakati zote asubuhi hadi usiku.
Mwalimu: Shule itakuwa na kompyuta, mtandao, na projektor. Mwanafunzi wa Mtwara atapata somo lilelile na wa DSM.
Daktari: Hospitali ya wilaya itafanya upasuaji usiku bila hofu ya umeme kukatika.
Kijana: Atapata ajira kwenye ujenzi, kwenye kiwanda, au ataanzisha biashara yake ya kusanikiza solar na umeme.
Mzee: Atapata pensheni yake kwa simu bila kwenda benki kwa sababu mitandao itakuwa imara.

ULINGANISHI NA NCHI NYINGINE
Nchi kama Ethiopia, Misri na China zilikua kiuchumi baada ya kumaliza miradi mikubwa ya umeme. Sisi sasa tunaingia kwenye klabu ya nchi zinazojitegemea nishati. Hii inatupa heshima kimataifa na inavutia wawekezaji kuipenda na kuja kuwezekeza Tanzania.
WITO NA DHAMANA ZETU
Ili tuweze kufanikiwa kila mmoja ana wajibu kama ifuatavyo:
1. Wajibu wa Serikali: Hakikisha umeme unafika maeneo yoyote nchini kwa gharama nafuu. Usipigwe na rushwa kwani zama tayari zimebadilishwa na serkali ya Dkt Samia na leo hii watanzania wanakwenda kuwa huru katika upatikanaji wa nishati ya umeme kwa uhakika.
2. Wajibu wa Sekta Binafsi na Wananchi: Njooni mwekeze. Anzisha kiwanda kidogo. Anzisha duka la kulea kuku. Tumia fursa huu ni mlango muhimu sana kwa wawekezaji wetu kuongeza mitaji lakini pia kufanya ubunifu mpya wa uwezekezaji utakakuwa na tija zaidi.
3. Wajibu wa Sisi Sote: Tulinde miundombinu hii. Huu ni utajiri wa wajukuu zetu. Tusiharibu kila mmoja atimize uzalendo wake kwa kulinda mradi huu kama mboni za macho ili uwe salama miaka na dahari.
Ni heshima kubwa isiyomithilika kwa Rais kipenzi chetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye uongozi wake lakini kwa watanzania kwa ujumla wake ambao leo wanashuhudia ndoto ya Nyerere ikitimia na ahadi ya Rais Samia imetimia na ikifanikiwa kwa zaidi ya 100% ambapo leo hii Tanzania imeanza safari mpya kupitia ujasiri na uthubutu wa mbeba maono Dkt Samia Suluhu Hassan.
Nimalizie kwa maneno ya Mwalimu Julius K. Nyerere “Maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe”. Serikali imetoa umeme. Sasa ni zamu yetu kutengeneza maendeleo yetu.
Asante Mhe. Rais Samia. Asante Serikali ya Awamu ya Sita. Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makala hii imeandikwa na Cde Shaka Hamdu Shaka DC Kilosa.

More Stories
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino
InnoIP Tanzania yazinduliwa kuimarisha ulinzi wa ubunifu
Ndejembi:Tanzania sasa inaziada ya Umeme Megawati 2375