May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yatarajia mafanikio makubwa Serikali ya awamu ya sita

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inamatarajio makubwa na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kutokana na jitihada mbalimbali ambazo imekuwa ikifanya ikiwemo ushirikiano katika mipango na mikakati mizuri ambayo imekuwa ikisaidia kuongeza mapato na kuleta tija katika Taifa.

Jenerali John Mkunda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam mapema leo hii wakati wa Uzinduzi wa mikondo miwili ya uzalishaji na muonekano mpya wa chupa za maji ya uhuru Peak pamoja na

Amesema Serikali imekuwa na matarajio makubwa na Jeshi la kujenga taifa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitembea kifua mbele kutokana na kuwa na chombo ambacho kinachotekeleza majukumu yake na kuiwezeaha nchi kuwa na amani.

“Matarajio yangu kwa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) ni makubwa na imani weledi mliokuwa nao katika kutekeleza miradi mikubwa imani yangu kwa Jeshi ni kubwa natumaini amtaniagusha kama ilivyo kuwa ada na kuendelea kutimiza wajibu wanu kama ilivyoada”alisema amesema Jenerali Mkunda
“Mnaweza kuona Serikali ilivyokuwa na imani na nyingi nichukue fursa hii kuwapogeza na matarajio yangu ni makubwa kwenu”amesisitiza Jenerali Mkunda.

Jenerali Mkunda amesema juhudi zinazofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT na Jeshi Kwa ujumla zimelenga kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za Biashara na Huduma katika Taifa kwa ujumla.

Amesema Mwezi Julai, kulizinduliwa mradi wa Kituo cha Mafuta na leo hii anazindua mikondo miwili ya uzalishaji na bidhaa mpya ya maji ya kunywa na kueleza yote hayo yanatokana na jitihada, ushirikiano, mipango na mikakati mizuri ambayo imekuwa ikisaidia kuongeza mapato na kuleta tija ndani ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) pamoja Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa ujumla

Aidha alitoa wito kwa Shirika kuendelea kubuni miradi mikubwa na kuboresha miradi na viwanda vilivyopo ili bidhaa zinazozalishwa ziweze kukidhi mahitaji ya ndani na nje ya nchi.

Pia aliwasii watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ufanisi ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea

“Nitoe rai kwa watendaji kutunza miundombinu ya Kiwanda hiki, ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora wa maji yanayozalishwa ili wateja wetu kote nchini waendelee kutumia na kufurahia maji haya ya kunywa ya Uhuru Peak na hivyo kuongeza mapato ya kiwanda”amesema

Awali Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema
Mitambo hiyo yenye mikondo miwili imenunuliwa na kufungwa, ambapo mkondo wa kwanza una uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo 350 mls na 600 mls (kawaida na premier), lita 1 na lita 1.6. huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha chupa 10,000 kwa saa.

Amesema kwa Mkondo wa pili unazalisha maji makubwa yenye ujazo wa lita 13 na lita 18 pamoja na kuwa na uwezo wa kuzalisha chupa 500 kwa saa.

“Bidhaa hizi zimefanyiwa utafiti wa soko ili kukidhi matakwa ya wateja wetu Sambamba na ununuzi wa mtambo hii, Shirika lilifanya ukarabati wa majengo, kuboresha maabara, miundombinu ya umeme na ununuzi wa magari mawili (3.5 Tones) ambapo vyote kwa pamoja vimegharimu kiasi cha TShs 1,839,495,507.75″amesema.

Aidha amesema azma ya Shirika ni kuhakikisha Kampuni na miradi yake mbalimbali inakua na kuongeza vyanzo vya mapato vitakayowezesha Shirika kutekeleza malengo yake kwa ufanisi zaidi.

Aidha amesema uzinduzi wa bidhaa hizo mpya utaongeza wigo katika sekta ya Biashara na Huduma na kuongeza wateja, na kuliwezesja Shirika kupata faida zaidi.

“Nitoe wito kwa Wakuu wa Kamandi, Vikosi, Shule, Vyuo pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutumia maji haya ya Uhuru Peak, kwani yana viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa”amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Hassan Mabena akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Ofisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele
amesema kiwanda hicho cha Maji ya Kunywa SUMAJKT Bottling Co Ltd kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na uwezo mdogo kiuzalishaji.

Amesema Hali hiyo ilipelekea Shirika kuweka mipango ya kuongeza Mikondo ya Uzalishaji ili kukidhi matakwa ya wateja wetu.

“Menejimenti ya Shirika chini ya Bodi ya Ushauri ilipitisha mapendekezo ya maboresho na hatimaye kuagiza mitambo itakayowezesha kuzalisha bidhaa mpya za maji ambayo ikikupendeza utaizindua leo hii”amesema