May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jk akutana na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo, Marekani

Na Mwandishi Wetu

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika mashindano ya marathon yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023. 

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Uchumi – wa Zanzibar na kushoto ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.

Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo. Rais Mstaafu amempongeza Gabriel Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. 

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo aliyeongozana na mwanariadha Gabriel Geay alipokutana nao mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.

Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo “Bongo Zozo”. Amewapongeza pia kwa kuhamasisha ushindi huu na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania juu. 

Rais Mstaafu yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia mpango wa uongozi wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program”. 

Katika mafunzo hayo, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Uchumi – wa Zanzibar ameshiriki pia.