Na Mwandishi Wetu
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika mashindano ya marathon yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023.
Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo. Rais Mstaafu amempongeza Gabriel Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo “Bongo Zozo”. Amewapongeza pia kwa kuhamasisha ushindi huu na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania juu.
Rais Mstaafu yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia mpango wa uongozi wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program”.
Katika mafunzo hayo, Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Fedha na Uchumi – wa Zanzibar ameshiriki pia.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango