November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera- Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, na pia Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma Jenista Mhagama (kulia), amechukua fomu ya kuwania tena jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mhagama amechukua fomu hiyo leo Julai 15, 2020 kwa kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini (kichama) Mohamed Lawa (kushoto). (Picha na Yusuph Mussa)

Jenista Mhagama achukua fomu kuwania tena jimbo Peramiho

Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Songea

ALIYEKUWA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera- Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, na pia Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, Jenista Mhagama amechukua fomu ya kuwania tena jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mhagama amechukua fomu hiyo leo Julai 15, 2020 kwa kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini (kichama) Mohamed Lawa ili kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu.

Mhagama ambaye pia alikuwa anaratibu shughuli za Bunge, na amekuwa akisimamia Sheria, Kanuni na Taratibu, huku akiwasaidia baadhi ya wabunge kuweza kufanya shughuli zao ndani ya Bunge kwa weledi, ni mmoja wa wanawake wa ‘shoka’ ambao wanapambana kwenye majimbo badala ya Viti Maalumu.

Baadhi ya  wanawake wengine wanaowania ubunge kwenye majimbo ni Mary Chatanda (Jimbo la Korogwe Mjini), Ummy Mwalimu (Jimbo la Tanga Mjini), Mwantumu Mahiza (Jimbo la Mkinga) na Mboni Mhita (Jimbo la Handeni Vijijini) mkoani Tanga. 

Wengine ni Mama Salma Kikwete (Jimbo la Mchinga mkoani Lindi), Anne Kilango (Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro) na Mary Nagu (Jimbo la Hanang’ mkoani Manyara).