November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jamii yatakiwa kulinda miradi ya wawekezaji wazawa

Na Esther Macha, Timesmajira Online,Songwe

JAMII imetakiwa kulinda na kutunza miradi inayowekezwa na wawekezaji wazawa katika maeneo mbalimbali nchini ili iweze kuwanufaisha wananchi na kuwainua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kijiji cha Masangula ,Diwani wa Kata ya Nyimbili Jimbo la Vwawa mkoa wa Songwe Tinson Nzunda ambaye ni Mwekezaji wa kampuni ya Lima amesema uwepo wa wawekezaji katika maeneo mbalimbali umekuwa na manufaa kwa wananchi .

Ameeleza kuwa wananchi wengi waliopo katika kijiji hicho maisha yao yanategemea ajira za muda mfupi kupitia uwekezaji aliofanya na kwamba hakuna mwananchi ambaye ataharibu miradi hiyo.

“Tunaomba serikali iendeleee kutuwekea mazingira rafiki wawekezaji ili tuendelee kufanya kazi kwa uhuru,”amesema.

Bonifasi Kibona ni mkazi Tunduma mkoani Songwe ambaye ni dereva katika kampuni hiyo huku kazi yake ni kupeleka miche ya kahawa kwenye mashamba na kazi zingine zinahusu shughuli za shamba.

Diwani kata ya Nyimbili na Mwekezaji wa Kampuni ya Lima Tinson Nzunda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari

Kibona amesema kupitia Mwekezaji huyo maisha yake yamebadilika kwani ameweza kusomesha watoto wake pamoja na kuendeleza kilimo nyumbani kwake pamoja na ufugaji wa mifugo mbalimbali .

Moja vipande vya miche ya Karanga