Na Raphael Okello,TimesMajira Online. Musoma
JAMII imeshauriwa kudumisha kanuni na taratibu za afya, hasa kunawa mikono kama ilivyokuwa wakati wa ugonjwa wa COVID-19, ikiwa ni hatua ya kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Florian Tinuga wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni mjini hapa kuwa kwa kipindi chote ambacho kanuni na taratibu za kunawa mikono kila wakati, zilisimamiwa hata milipuko ya magonjwa mengine ya kuambukiza ilipingua.
“Kanuni ya kunawa mikono katika suala la kujikinga na magonjwa ya milipuko kama kuhara, kipindupindu na magonjwa mengine ya tumbo zinatakiwa kuzingatiwa kila wakati,” amesema.
Ameongeza; “Takwimu zetu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha COVID-19, kiwango cha maambukizi ya magongwa ya kuhara na magonjwa mengine ya tumbo kimepungua kuliko vipindi vingine,” alisema.
Kwa upande wake, John Wambura mkazi wa mjini Musoma akitoa maoni yake kwa Majira amesema serikali, inatakiwa kutoa elimu kwa kuijengea jamii tabia ya kufanya usafi inayoambatana na kunawa mikono kila mara.
More Stories
Huduma ya kusafisha figo yasogezwa Manyara
Rais Samia aandika historia barani Afrika
Mapambano dhidi ya Marburg waandishi watakiwa kuelimisha jamii