May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mganga Mkuu wa mkoa Iringa Dkt. Robert Salim pamoja na Meneja wa mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt Dafrossa Lyimo .

Iringa yafanikisha upatikanaji wa Chanjo

Na Esther Macha,TimesMajira,Online Iringa

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Iringa ,Dkt.Robert Salim amesema kwa kushirikiana na serikali na wadau wamewezesha upatikanaji wa chanjo zote za kuzuia magonjwa yanayozuilika ili kuweza kuepusha vifo .

Ametaja magonjwa yanayolengwa  na mpango wa  Taifa  wa chanjo kuwa  ni kifua kikuu ,Dondakoo,kifaduro ,polio,surua ,Rubella,Pepopunda,Homa ya ini,homa  ya uti wa mgongo,kichomi,kuhara na saratani  ya mlango wa kizazi .

Pia amesema wameweza kufika kiwango cha uchanjaji kwa asilimia 99,ambayo ni hatua kubwa iliyofikiwa kwa serikali ya awamu ya tano katika kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Akifungua semina  ya siku moja kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi  wa kinga  Wizara ya afya ,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Robert Salimu amesema hayo hivi karibuni katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya,Iringa,Njombe,pamoja na Ruvuma.

Dkt.Salim amesema kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli  kwa kushirikiana na shirika la Gavi,wadau na wadau wengine wa maendeleo imefanikiwa kununua magari 74.

Ametaja  aina ya magari hayo kuwa ni Fork lift tatu ,generate moja vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.Bilion 7 kwa ajili ya kuimarisha huduma za chanjo hapa nchini.

Amesema kuwa kati ya magari 74 yaliyonunuliwa magari 61 ni aina ya Toyota Pickup ambayo kila moja ina thamani ya sh.milioni 56.6 kwa ajili ya kuimarisha usambazaji wa chanjo katika halmashauri 61hapa nchini.