Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MKUU wa Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof.Hosen Mayaya ameeleza mafanikio lukuki yaliyochangiwa na Baraza la Wafanyakazi la Chuo hicho.
Akizungumza katika uzinduzi wa Baraza jipya la chuo hicho ambalo limemchagua Stellah Masanja kuwa Katibu na Christian Makupa kuwa Katibu Msaidizi Prof.Mayaya amesema mafanikio hayo ni kutokana na utekelezaji mzuri wa majkumu ya Baraza la wafanyakazi lililopita.
Prof.Mayaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo ameyataja mafanikio hayo kuwa ni nm pamoja na kuongezeka kwa udahili na usajili wa wanafunzi Chuoni kutoka wanafunzi 14,252 hadi wanafunzi 14,428,kuongezeka kwa idadi ya wahitimu kutoka wahitimu 8,182 hadi wahitimu 8,918,kufanya marejeo ya kuhuisha mitaala 15 na kuanzisha mitaala mipya saba ,kuongezeka kwa tafiti zinazofadhiliwa na Chuo kutoka tafiti saba zenye thamani ya shilingi milioni 84.0hadi kufikia tafiti 16 zenye thamani ya shilingi milioni 240 kwa mwaka 2022/2023.
Aidha ametaja mafanikio mengine kuwa ni miradi ya tafiti shirikishi mitano yenye thamani ya shilingi 6,606,427,555 ilitekelezwa,kuongezeka kwa Mapato ya Ndani ya Chuo kutoka shilingi bilioni 16.360 hadi kufikia shilingi bilioni 23.406 sawa na ongezeko la asilimia 43,kuongezeka kwa watumishi kutoka 252 hadi kufikia watumishi 430,kuweka mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia kwa kuongeza nafasi mpya zikiwemo nafasi 110 za ofisi, nafasi za malazi kwa wanafunzi 1,014, nafasi 4,554 za wanafunzi kukaa wakati wa masomo kwa mara moja na kujenga mgahawa yenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja.
Vile vile amsema,baraza hilo limefanikisha kujenga Maktaba kubwa yenye uwezo wa kuhudumia watumiaji 600,kununua ekari 696.71 kwa ajili ya upanuzi wa Chuo eneo la Chigongwe/Nala,kulipa madeni kwa wazabuni na wafanyakazi wa Chuo kiasi cha shilingi 3.068 kati ya shilingi bilioni 3.079 deni lililokuwa la siku nyingi .
Prof.Mayaya amesema,chuo hicho pia kinaendelea kupata hati safi za ukaguzi wa hesabu za Chuo kwa mwaka wa fedha,kupata tuzo ya mshindi wa kwanza ya usimamizi bora wa rasilimaliwatu katika kundi la vyuo vya elimu ya kati na vyuo vya elimu ya juu,kushinda tuzo ya Kitaifa ya waandishi bora wa ‘Article’ ya kisayansi katika “Journal”bora za Kimataifa; na kushinda nafasi ya tatu katika tuzo za uwezeshaji wananchi kiuchumi inayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Aidha amezungumzia miradi inayotarajiwa kutekelezwa na chuo hicho katika mwaka wa fedha 2023/2024 ni pamoja na miradi ya ujenzi wa jengo la utawala katika eneo la Mbwanga Kampasi kuu Dodoma, ujenzi wa bweni la wanafunzi katika eneo la Kitumba Magu Mwanza na jengo la Taaluma linalofadhiliwa na mradi wa HEET litakalojengwa katika eneo la Miyuji Kaskazi hapa Dodoma.
Prof.Mayaya ametumia nafasi hiyo kuisgukuru serikali ya Awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kukijengea uwezo Chuo na hivyo kuwa na mazingira rafiki na wezeshi.
Akifungua mkutano wa Baraza hilo jipya ,Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Natuel Mwamba amekipongeza chip hicho kwa mafanikio hayo makubwa .
“Mimi nimeshakuwa katika taasisi zba Elimu ya Juu,kwa hiyo kwa haya mliyoyaeleza ,chuo kipo vizuri na kwa dhati ya moyo wangu nawapongeza kwa sababu najua ana mafanikio haya mmepambana sana.” Amesema Mwamba
Aidha amelitaka Baraza hilo jipya la wafanyakazi kuwa makini kwenye vikao vyako na kuwasemea wanaowawakilisha na kuwapa mrejesho wa mambo ambayo hawayaelewi vyema.
“Baraza la wafanyakazi ni jicho , siko na Mdomo wa wengine hivyo mnapaswa kuwasemea mambo yao bila kufanya hivyo hamtawatendea haki.”amesisitiza
Aidha Katibu Mkuu huyo amewataka wajumbe wa Baraza hilo wasome sheria ,kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali ili kufanya kazi kwa Weledi na hivyo kuongeza tija kwa wafanyakazi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua