Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
OFISA Maendeleo Vijana,Uratibu na Uwezeshaji Vijana Kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu,Nassibu Mwaifunga amezindua ilani ya vijana ya mwaka 2020 hadi 2025 ambayo imebainisha mambo mbalimbali zinazowakabili vijana nchini.
Akizindua ilani hiyo,leo katika mkutano wa siku tatu wa zaidi ya vijana 300 kutoka mikoa mbalimbali,Mwaifunga amesema uzinduzi wa Agenda ya Vijana ya Mwaka 2020-2025 ni muhimu kwa kuwa inachochea upatikanaji wa huduma na mahitaji mbalimbali ya vijana.
” Kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi na vijana ni kundi kubwa kwenye jamii ni muhimu vijana kuwa na Agenda ambayo itasaidia kuchochea upatikanaji wa maendeleo shirikishi na endelevu katika Nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi,”amesema na kuongeza
“Agenda hii ni nyenzo muhimu ya ushawishi katika kuwahabarisha wagombea,Serikali, vyama vya siasa, washirika wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia juu ya mchango wa vijana katika kutatua changamoto za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa kuwashirikisha ipasavyo,”amesema
Amesema utayarishaji wa agenda hiyo umezingatia Malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ambayo ni sawa na Vipaumbele vya vijana vya agenda hii baada ya kukusanya maoni na kuyachakata katika maeneo makuu matano Elimu , Afya, Ajira,Uongozi(Ujumuishwaji) na taarifa.
” Agenda hii inatarajia kuongeza kasi ya kutafsiri utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana kwa vitendo na kutatua changamoto za vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi yetu,”amesema
Mwenyekiti wa Mashirika 13 yaliyoandaa agenda ya Vijana 2020 -2025,Rogers Fungo amesema safari ya uandaaji wa ilani hiyo ilianza mwezi Februari mwaka huu kwa mashirika 13 ya vijana.
Amesema ilani hiyo ya vijana inatoa taswira ya hali ilivyokuwa sasa kwa kuonesha juhudi zinazochukuliwa,fursa na changamoto zilizopo kwa vijana.
Ametaja baadhi ya mashirika yaliyoandaa Agenda hiyo ni pamoja na Tanzania Bora Initiative(TBI),Tanzania Youth Coalition(TYC),Tanzania Youth Vision Association (TYVA),United Nation Association (UNA),Restless Development,Youth Partnership Countrywide(YPC),Youth of United Nations Association of Tanzania (YUNA).
Amesema nyingine ni African Youth Transformation (AYT),Poverty Free and Community Empowered Foundation
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam