May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

IGP Wambura awaapisha maofisa waliopandishwa vyeo na Samia

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MAOFISA wa Jeshi la Polisi 155 waliopandishwa vyeo na Rais Samia Suluhu Hassan, wamekula kiapo cha utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na kiapo cha maadili ya viongozi wa umma.

Maofisa hao ambao ni makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi, wapo 27 waliopanda vyeo kuwa manaibu kamishna.

Pia wamo makamishna wasaidizi wa Polisi ambao wamekuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi, ambao ni 128.

Akitoa nasaha  Februari 19, 2024 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura amesema, kupandishwa vyeo kwa maofisa hao, kutaongeza chachu ya utendaji kazi, kutenda haki, uadilifu na nidhamu pia wananchi wategemee mabadiliko makubwa ya kiutendaji.

 Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Susan Kaganda amesema miongoni mwa waliopandishwa vyeo, wapo maofisa wanane wa kike, ambao wamepanda vyeo na kuwa manaibu kamishna wa Polisi.

Akizungumza kwa niaba ya waliopandishwa vyeo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi David Misime amesema kupanda kwao vyeo, kutaongeza morali na utimamu zaidi wa akili katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi.