Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online, Nairobi
JUMUIYA ya Mawasilianoya Afrika (ATU) imetia saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na kampuni kubwa ya teknolojia ya Huawei ambayo itahakikisha nchi na mashirika ya Kiafrika yanajenga uwezo kwa ajili ya mabadiliko ya TEHAMA.
Katika makubaliano hayo, Huawei itatoa mafunzo ya kukuza ujuzi wa kidijiti na kuhakikisha mashirika hayo mawili yanashirikiana kusaidia ubunifu wa ndani, kubadilishana habari juu ya mwenendo wa mambo, changamoto na suluhisho kwa Afrika na ulimwenguni huku ikipanua uchumi wa kidijiti pamoja na unganisho la vijiji kupitia utafiti.
Hatua hiyo inakuja, huku ripoti ya 2019 ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) juu ya uchumi wa kidijiti ikionesha kuwa Afrika na Amerika ya Kusin kwa pamoja zinachangia chini ya asilimia 5 ya vituo vya data ulimwenguni.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kwamba ikiwa suala hilo litaachwa bila kushughulikiwa, kutakua na ongezeko katika mgawanyiko wa usawa wa mapato uliopo sasa.
“Hii, ikijumuishwa na ukweli kwamba katika nchi zinazoendelea (LDCs), ni mtu mmoja tu kati ya watano anayetumia mtandao (internet) ikilinganishwa na watu wanne kati ya watano katika nchi zilizoendelea,” imeeleza ripoti.
Akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini iliyofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya, katika makao makuu ya ATU, John Omo, Katibu Mkuu wa ATU, aliipongeza kampuni ya Huawei kwa mchango wake barani Afrika.
“Huawei imebadilisha muunganiko na imetoa mchango mkubwa barani Afrika kupitia uwekezaji wake katika miundo mbinu ya kidijiti ambayo ni rafiki kwa mazingira, kutoa ufundi wa ICT pamoja na teknolojia za hali ya juu kwa maeneo ya vijijini.
Shirika hili ni mshirika wa maendeleo anayeaminika barani Afrika. Makubaliano tunayo saini yanalenga kuimarisha ushirikiano huu,”alisema na kuwa Afrika ina nafasi kubwa ya kunufaika kutokana na teknolojia mpya.
Mashirika hayo mawili yana historia ndefu ya kufanya kazi pamoja na makubaliano hayo mapya yatasaidia nchi za Kiafrika, wasimamizi, na raia kufaidika na mabadiliko ya uchumi wa kidijiti, kuhamia kwa teknolojia mpya, kukuza mitandao salama na kupata ujuzi wa kidijiti unaohitajika ili kusukuma uchumi mbele.
Samuel Chen, Makamu wa Rais wa Huawei Kusini mwa Afrika,aliishukuru ATU kwa uongozi na uendelezaji wa ICT barani Afrika:
“ATU inachukua jukumu muhimu kusaidia nchi wanachama katika sera na mikakati yao, kusaidiana uzoefu, kujenga uwezo na kuendesha ubunifu na tunafurahi kuweza kuwaunga mkono.” alisema.
“Tumeunganisha mamilioni ya Waafrika katika huduma salama, za kasi,na za mtandaoni katika kipindi cha miongo miwili iliyopita na kupata uaminifu na msaada wa wateja wetu na wasimamizi.Tunatarajia kufanya hata zaidi.” aliongeza
Kulingana na makubaliano hayo, washirika wataanza kutoa mafunzo kwa ATU ambao watapata nafasi ya kushirikiana na wataalam kutoka kote ulimwenguni kujadili teknolojia na mwenendo wa mambo pamoja na kushirikiana kwenye utafiti kusaidia maendeleo ya kidijiti barani Afrika.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati