May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya yaanzisha kituo cha malezi kwa watoto

Na Esther Macha, Timesmajira, Online,Mbeya

HOSPITALI ya Rufaa kanda ya Mbeya imeanzisha kituo cha uangalizi wa watoto wadogo wa watumishi wa hospitali hiyo kuanzia 0 mpaka miaka mitatu lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto za watumishi kukimbiwa na wasaidizi wa nyumbani hivyo kupata sabababu za kuchelewa kufika kazini .

Imeleezwa kuwa pia uwepo wa kituo hicho pia utasaidia usalama wa watoto wa watumishi kulelewa vizuri ikiwa ni pamoja na kulinda usalama wao pindi watumishi wanapokuwa makazini .

Akizunguma Timesmajira jana Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji katika kuelezea ubunifu ubunifu ambao alisema utasaidia kuongeza ufanisi katika kazi kwa watumishi ,pia itasaidia kupunguza ruhusa kwa watumishi.

“Kwa ubunifu huu kigezo cha kundokewa au kutokua na dada wa kazi au kuchelewa kufika kazini kwa kwa watumishi kipindi anapokosa mwangalizi wa kumwachia motto nyumbani haitakuwa changamoto tena nah ii itawafanya watumishi wote wenye watoto wadogo kufanya kazi kwa uhuru na bila hofu baada ya uwepo wa kituo hiki “amesema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo Dkt. Mbwanji ameeleza kuwa kituo hicho ambacho kipo eneo la hospitali kitakua nawaangalizi wa watoto wenye taaluma hiyo ikiwemo ya uwalimu ambapo wazazi(watumishi) watapata fursa ya kwenda kumuona mtoto kwaajili ya kumnyonyeshana pale inapofika muda kazi kuisha, mzazi atapata fursa ya kumchukua mtoto wakena kurudi nae nyumbani.

Akielezea zaidi Dkt. Mbwanji amesema kuwa kikubwa ni kwamba mtoto anakuwa salama na inasaidia kuongeza tija katika utendaji kazi kwa watumishi na watoto watapata fursa yakufundishwa, kucheza michezo mbalimbali ya watoto, kupumzika (vitanda vya kulala)na tv zenye kuonyesha katuni zenye mafunzo kwa watoto.

Wakieleza furaha yao baada ya uanzishwaji wa kituo hicho felister Saria na Daniel Kajane watumishi wa hospitali ya rufaa ya kanda mbeya wameelezea furha yao na kushukuru uongozi wa hospitali kwa ubunifu huo ambaoutawasaidia watumishi katika usalama wa watoto na wao kufanya kazi kwa juhudi kwakuondoa kikwazo kilichokuwepo.

“Kwa sisi watumishi uanzishwaji wa kituo hiki umekuwa msaada mkubwa kwani watumishgi tulio wengi tumekuwa na changamoto ya kutokuwa na wasaidizi wa nyumbani hivyo kupelekea kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kuishia muda mwingi kuomba ruhusa hivyo kazi nyingine kushindwa kufanyika kwa wakati ,uwepo wa kituo hiki naamini itakuwa msaada mkubwa sana kwanza kipo ndani ya hospitali yetu hata kwa watumishi wanaonywesha hawatapata shida tena kwani ujirani pekee wa kituo utakuwa ufanisi tosha wa kazi”amesema mmoja wa watumishi wa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Ferister.