January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospitali ya Aga Khan waadhimisha siku ya kimataifa ya Fiziotherapia


Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Hospitali ya Aga Khan imeadhimisha siku ya kimataifa ya Fiziotherapia lengo ikiwa ni kutatua tatizo la maumivu ya mgongo (LBP) Ili kuimarisha afya pamoja na mijongeo ya mwili na viungo.

Akizungumza na waandishi wa Habari juzi wakati wa madhimisho hayo ambayo huadhimishwa kila mwaka siku ya tarehe  8 Septemba, Mfuziotherapia kutoka Hospitali ya Aga Khan, Simon Gundah alisema wamefanya kambi ya uchunguzi wa bure kwa wote wenye maumivu ya mgongo na kutoa elimu ya bure kwa washiriki kuhusu maumivu ya mgongo na namna ya kuyadhibiti.

Pia alisema washiriki hao walipatiwa ushauri wa bure na kupatiwa mpango wa matibabu kwa punguzo la hadi 50%•

“Hospitali ya Aga Khan inajitolea kutoa huduma maalum za kitaalamu ili kusaidia kuboresha afya katika jamii, kupitia uelimishaji kuhusu mikakati y akudhibiti maumivu ya mgongo, kuweka mipango maalum ya mazoezi ya viungo na matibabu ya fiziotherapi” Alisema 

“Matatizo ya maumivu ya mgongo ni matatizo makubwa kwa afya duniani likiwaathiri takribani takribani watu milioni 619 mwaka 2020 na pia ni chanzo kikuu cha ulemavu, tatizo hili linaweza kumuathiri mto yeyote na mara nyingi haliwezi kubainishwa kwasababu moja inayojulikana” 


Pia Gundah aliendelea kwa kusisitiza umuhumu wa Fiziotherapia katika kutibu na kudhibiti maumivu mbalimbali ya viungo

“Fiziotherapia ni ufunguo wa kuishi bila maumivu ya viungo ambapo uimara wa migongo yetu unasaidia nguvu za maisha yetu”

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa Hospitali hiyo, Murtaza Muktali alisema maumivu na wagonjwa wenye matizo hayo yanaongezeka kila siku ambao takwimu zinaonyesha karibu wagonjwa zaidi ya 20 kwa siku  wenye matatizo hayo ikiwa ni sawa na asilimia 80 wamekuwa wakifika katika hospitali hiyo 

“Huko nyuma wazee ndiyo walikua wakiongoza kwa magonjwa haya ya mgongo lakini kwa sasa hivi tunaona hata vijana wanaathirika na shida ya mgongo, hii ni kwasababu vijana wengi ambao wanafanya kazi wanakuwa hawana elimu ya jinsi ya kukaa kwa muda mrefu ofisini kwasababu ukikaa ofisini kwa muda mrefu haya matatizo yanatokea”

“Pia sababu nyingine ya watu kupata matatizo haya ni kwasabahu ya uzito wa kupitiliza, tatizo hili la mgongo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, madaktari na wafizithioropia ni lazima na ni muhimu kuelewa na kujua umuhimu wao lakini pia kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kukaa ofisini” Alisema 



Naye Emmanuel Mtui kutoka Kampuni ya Sun Pharmaceuticals alisema wameungana na Hospitali ya Aga khan kutoa elimu katik suala la maziezi tiba ambayo yansababishwa na maumivu ya mgongo na mungio 

“Wakati daktari anapotibu kuna hatua ya mwisho ambayo anatoa dawa ili kumsaidia mgonjwa kuendelea kupata nafuu, sisi tuna dawa yetu ambayo mgonjwa ataitumia na kuendelea kupata nafuu zaidi hivyo sisi kama kampuni tuna kuwa kama sehemu ya kutoa dawa ambazo zinahusiana na maumivu anayoyapata mgonjwa anbaye tayari ameshatibiwa na daktari”

Nivad Nziku kutoka Kampuni ya troikaa alisema wameshirikiana na madaktari wa Aga Khan ili kuwapa elimu wagonjwa inayohusiana pamoja na dawa zao ambapo  wanazitoa kwa wagonjwa hao ambapo  huwa zinawasaidia kuondoa maumivu kwa haraka.